Tanzania Association of Wichita

Membership Renew

Enter Amount:

Subscribe

KESHO: SOCCER: Wichita FC vs Houston FC in Wichita!!!!! PDF Print E-mail
Written by MushiPc   
Friday, 28 October 2011 20:05

UPDATES:

Kwa mujibu wa Wichita PD, Basi la kwanza kutoka Houston limewasili mchana huu kimya kimya likiwa na timu nzima pamoja na "kamati ya ufundi". Wameshapata kibali cha kuutumia uwanja usiku wa leo kwa jaramba la kuchangamsha misuli katika kujiweka katika hali ya kuonyesha kandanda murua kesho kuanzia saa kumi unusu kwa saa za kwetu.

Kapteni wa Wichita FC, beki wa kati D1 Cheche anahimiza wachezaji wake kufika mapema kesho, anatangaza uzi mahsusi wa kesho ni wa rangi ile ya Man City walipomnanihii Man U weekend iliyopita, na anahimiza mashabiki wa soka mvalie rangi hizo kama sapoti ya timu yenu.

Kipyenga kitapulizwa 4:30pm CT sharp!!

Mambo Entertainment kama kawa, wamejiweka sawa tayari kuwatoa kibaridi wapenzi wa soka katika ukumbi wao nyumbani Touch Of Class with a Halloween Party of the Decade!!!. CEO wa Mambo Entertainment, Bwimbo Wa Kajanja anasema Mtu Mzima Hatishiwi Nyau na kama unamatatizo ya Moyo, pata ushauri wa daktari kabla ya kuingia kwenye Halloween Party hii, wamejiandaa kuacha gumzo!!

Tukutane uwanjani REDBUG PARK (21st and N Edgemoor St)

    MwanaTaWichita,

    Ile Timu yenu ya mahiri ya soka, Wichita FC iliyokuwa imeweka kambi kabambe nje kidogo ya mji,  inafuraha kuwatangazia kwamba imerudi mafichoni na inakukaribisha kushuhudia kabumbu la hali ya juu wakati watakapowakaribisha mahasimu wao wa jadi kutoka Houston TX Jumamosi Oktoba 29 kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Redbud Park (21st and N Edgemoor St) kuanzia kumi na nusu jioni kwa saa za Wichita(4:30pm CT)

    Meneja wa Timu Mazaza Wa Mtawali (aka B.I.G) anaripoti vijana wake wapo fiti, wenye afya njema na nidhamu ya hali ya juu. Mazaza anasema anawakati mgumu sana mwaka huu wa kupanga kikosi kitakachovalia uzi wa kuichambua Houston kutokana na uchu walioonyesha vijana wakati wa maandalizi ya mechi hii. Kapteni wa Wichita FC Diwani Cheche ameahidi ushindi mnono na kuundeleza uteja wa Houston FC mbele ya vijana wa Wichita.

    TaWichita inaona ni vyema tukakumbushana mambo yalivyojiri ilipokutana miamba hii.

    2008 Summer: Venue Wichita, matokeo 1-2 Houston FC
    2008 ThanksGiving: Venue Houston: Mpira uliahirishwa sababu ya mvua
    2009 Summer: Venue Wichita, 2-0 Wichita FC
    2010 Summer: Venue Wichita, 3-1 Wichita FC
    2011 Oct 29: Venue Wichita<< USIKOSE>>

    Kwa habari zaidi, t'fadhali wasiniana na Kapteni Cheche 316-300-0043.

    TaWichita inawakaribisha kwa moyo mkunjufu wa "Mgeni Njoo..." ndugu zetu wa Houston FC, na wapemichezo wote wa Wichita na vitongoji vyake kwenye "shughuli" hii mwisho wa mwezi huu. Tunauhakika chama letu la Wichita FC litaibuka kidedea, kama kawa!

    UONGOZI

 

Add comment


Security code
Refresh

Lives changed by a text message

When cooking can be deadly