Tanzania Association of Wichita

Membership Renew

Enter Amount:

Subscribe

RESULTS! SOCCER Game Wichita FC vs Houston FC in Wichita!!!!!‏ PDF Print E-mail
Written by MushiPc   
Thursday, 03 November 2011 22:01

2011 Soccer

 

MwanaTaWichita,

Wapenzi wa michezo walishuhudia soka zuri la kuvutia jana jioni kwenye viwanja vya Redbug Park, kati ya mahasimu wa jadi, Houston FC na wenyeji wao Wichita FC.

Ikianza na fomesheni ya 4-4-3 Houston FC walionyesha nia yao ya kulipiza kisasi cha kusalimu amri mara mbili mfululizo kwa kuanza kwa kasi na gonga maridhawa ambazo ziliwazimisha wenyeji wacheze kwa kujihami na mashambulizi ya kushtukiza, na wapenzi wa Wichita FC wameze mate kwa tabu. Iliwachukua wageni dk kumi na mbili kuandika bao la kwanza na kuongeza la pili dakika nane baadae.

Wichita FC ilizindika na kulazimisha mashambulizi makali na kurudisha bao moja kupitia kwa Douglas kufuatia sekeseke golini kwa Huston FC baada ya mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi na midlefield Ngassa.
Dakika chache kabla ya mapumziko foward ya Houston ilitaka kuleta presha nyingine langoni mwa Wichita ambapo ilimlazimu nyanda nambari moja Peter Munisi kukifuata kitu kilichokuwa kinaelekea juu angle 90 ya goli lake na kupangua kabla mabeki wa Wichita hawajaondoa hatari ile.

Wakati kipyenga cha mapumziko kinapulizwa, ubao wa matangazo ulikuwa unasomeka 1-2, Houston. Houston walidominate kipindi cha kwanza kwa umahiri mkubwa.    

Meneja wa Wichita FC Mazaza wa Mtawali (Kamanda) na msaidizi wake Moses (Uncle) walifanya kazi ya ziada ya kutuliza munkari uliojitokeza, pamoja na kubadilisha mbinu za kuipenya mgome ya Houston FC ambayo ilicheza kwa nidhamu ya hali ya juu.

Mabadiliko hayo yalirudisha uhai kipindi cha pili kilipoanza. Middle field za Wichita ambazo zilizalimika kurudi nyuma kusaidia mabeki kutokana na kasi ya vijana wa Houston ziliifuata fomashen change ya mameneja wao Mazaza na Uncle na kusababisha Huston wapunguze kasi.

Shambulizi la kushtukiza la Houston FC lilisababisha penalti baada ya beki mmoja wa Wichita FC kunawishwa mpira ndani ya kumi na mbili. Referri alihesabu maguu kumi na mbili na namba nane wa Houston bila ajizi na kwa ustadi mkubwa aliupeleka mpira nyavu mdogo na kumuacha nyanda Peter Munisi akiusindikiza kwa kwa jicho baya. Houston 3 Wichita 1.

Wakicheza kama mbogo mwenye jeraha la mkuki, Wichita FC walilishambulia lango ya Houston FC kama nyuki na kufanikiwa hatimaye kufanukiwa kuzitikisa nyavu za Houston kwa mara ya pili kwa shuti kali la kimo la mtoto mchanga kupitia kwa winga wao aliyeingia kipindi cha pili Shahari. Winga Shahari mwenye record nzuri ya kupiga magoli aliyemegewa pande la kisigino na Sugar ndani ya box na hakurembesha mpira ule.

Kuingiia kwa bao hili kulilazimisha Houston kurudisha majeshi nyuma ili kuhakikisha wanarudi kwao na ushindi huku wakitumia winga zao kwa mashambulizi ya kushtukiza ambao waliipa ngome ya Wichita iliyokuwa chini ya Kapteni D1 Cheche kazi ya ziada.

Foward mahiri wa Wichita FC, Iddy Ligongo ambaye bado anakumbukwa na Houston kwa bao mbili alizowapiga mwaka jana, aliufumani mpira nje kidogo ya box na kufumua shuti kali lilimpita nyanda wa Houston na kuwainua mashabiki wa Wichita FC. Shuti hilo likagonga mtambaa panya na kurudi uwanjani na kuokolewa na mabeki wa Houston.

Kipyenga cha dk 90 kilipopulizwa ubao wa magoli ulikuwa unasomeka Wichita FC 2 Hoston FC 3!

Tunazipongeza timu zote mbili kwa kuonyesha soka maridadi, na kipekee Houston FC kwa kusafiri na kuja Wichita TaWichita na wapenda michezo wote wanawaombea safari njema back to TX.

Mechi ijayo itakuwa Thanks Giving Weekend wakati ambapo Houston FC watakapoikaribisha Wichita FC in TX.

TaWichita inawapongeza Suzzy, Bwimbo na menejementi nzima ya Mambo Entertainment kwa kuwaburudisha wageni wetu kwenye Halloween Party.

Last Updated on Thursday, 03 November 2011 23:55
 

Add comment


Security code
Refresh

Lives changed by a text message

When cooking can be deadly