Tanzania Association of Wichita

Membership Renew

Enter Amount:

Subscribe

UANACHAMA WAKO KWA MWAKA 2011 PDF Print E-mail
Tuna imani kwamba wote tupo salama, na hatukudhuriwa na hali hii ya baridi kali na barafu iliyotukumba wiki hii. Ni suala la kumshukuru Mungu.

Tunachukua muda huu kuwashukuru wote ambao wameshaanza kutoa michango yao ya uanachama kwa 2011, pongezi za dhati. Tunatoa msisitizo kwa wale ambao hawajafanya hili, kujitahidi kutoa michango yao kufikia mwisho wa mwezi wa pili, i.e. Jumatatu ya tarahe 28.

Ada ya uanachama bado ni ile ile, $30 (single) na $50 (couples).

Mwaka wa uanachama ni January-December.

Kwa kutambua kwamba kila mmoja wetu ametingwa na majukumu mbalimbali, uongozi wenu umeandaa njia mbadala ambazo tuna imani zitakuwezesha wewe kuweza kufikisha mchango wako kwa ufanisi na haraka.

Unaweza tumia njia zifuatazo kulipia uanachama wako:

1. Kwa kupitia PayPal Account: Gonga Hapa (Tumia jina lako rasmi na e-mail address unayopokea nayo e-mail za chama kwa uhakiki wa Mtunza Fedha)

2. Kwa kupitia Bank Account yako ya TaWichita, Meritrust Credit Union Acct No: 08007955. Jina ni Tanzania Association of Wichita.

-Kwa tawi lililo karibu na wewe; Gonga Hapa

-*TUNZA RISITI yako kutoka Meritrust Bank kwa uhakiki ili upatiwe stakabadhi yako ya malipo ya uanachama 2011

3. Kwa kupitia kiongozi yeyote wa Chama. Kwa majina ya Viongozi wa awamu hii Gonga Hapa:

Ni haki yako kudai stakabadhi ya malipo yako ya uanachama. Wasiliana na kiongozi yeyote wa TaWichita au e-mail This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it kuhakikisha unapatiwa stakabadhi ya malipo yako.

Tuna imani njia hizi zitakuwezesha mwanajumuia kuweza kuwasilisha mchango wako. Tumejiwekea malengo ya kumaliza zoezi hili kufikia mwisho wa mwezi wa pili, yaani Jumatatu Februari 28, 2011.

Tunajiandaa kwa mkutano wa kwanza kwa 2011. Wiki chache zijazo tutabandika tangazo kwenye toviti yetu ambapo utapata nafasi ya kupiga kura siku ambayo utapenda mkutano ufanyike. Tarehe itakayopokea kura nyingi katika maoni hayo ndiyo itatangazwa kuwa siku ya mkutano wetu wa kwanza kwa 2011.

Tunatanguliza shukrani za dhati.

UONGOZI.

 

Add comment


Security code
Refresh

Lives changed by a text message

When cooking can be deadly